Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live.
Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Ali Kiba akizidi kuitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
Mwanamuziki Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live usiku huu.
Nyomi ikimpa shangwe Msaga Sumu.
Msaga Sumu akizidi kuwachizisha mashabiki wake.
Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic wakilishambulia jukwaa la Dar Live usiku huu katika shoo ya Mwana Dar Live.
Isha Mashauzi akifanya yake stejini.
Jay Millions (kulia) akimkabidhi Shamila Ramadhani (kushoto) mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 alizojishindia kupitia shindano la Jay Millions. Katikati ni mume wa Shamila.
Mshindi wa milioni 10 za Jay Millions, Shamila Ramadhani na mumewe wakionesha mfano wa hundi ya fedha hizo.
Jay Millions akipozi na baadhi ya wadau wa Dar Live sambamba na warembo alioambatana nao baada ya kutoa mahela kwa Shamila.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Pamela Daffa 'Pam D' akiwarusha mashabiki wa Dar Live kwa songi lake kali la Nimempata.
Post a Comment