Featured
Loading...

PICHA..!10 WAKUTWA NA SILAHA, MABOMU NA BENDERA YA ALSHAABAB.! BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAO





Morogoro. Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14 mwaka huu) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.

Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.

Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.

“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka,”

Alisema polisi waliendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni. Na mmoja kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumjeruhi askari mmoja na panga.

Name:  gaidi2.png
Views: 0
Size:  218.4 KB

Name:  Gaidi1.png
Views: 0
Size:  246.3 KB
Name:  gaidi3.png
Views: 0
Size:  231.1 KB

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright journal-bm | Designed By Code Nirvana
Back To Top